NAFASI ZA AJIRA: - MADEREVA
Kampuni: GIN INVESTMENT LIMITED
Mahali: DAR ES SALAAM – TANZANIA
Nafasi: 6
Kuhusu Sisi: GIN INVESTMENT LTD ni Kampuni binafsi ya Usimamizi wa Taka yenye leseni ya Manispaa ya kukusanya Taka ngumu na ada za usafi wa Mazingira kutoka kwa Mashirika ya Serikali na yasiyo ya serikali, Balozi, Kaya, Taasisi za kibinafsi na biashara
Majukumu Muhimu:
- Kuendesha magari ya Kampuni kwa ufanisi na usalama
- Kufanya ukaguzi wa gari kabla na baada ya kazi na kutoa taarifa ya haraka ya matengenezo ya gari kwa Msimamizi wako
- Kufuata kwa umakini sheria zote za barabarani, kanuni za usalama na sheria za Kampuni
- Kuwakilisha kampuni kwa ustaarabu katika mawasiliano yeyote na wateja
- Kuhakikisha vifaa muhimu vya gari kama spare tyre, kadi ya gari, fire extinguisher, jeki/toolbox vinatunzwa vizuri
- Kujaza logsheet kila trip au safari
Sifa:
- Leseni ya Udereva ya Tanzania; Madaraja C na E
- Uzoefu usiopungua miaka 5 ya udereva kitaalam
- Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Cheti halali cha Udereva kutoka VETA / NIT
- Uthibitisho wazi wa leseni ya udereva kutoka Traffic Police
- Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea na kama sehemu ya timu.
Jinsi ya kutuma maombi:
• Barua ya maombi pamoja na wasifu wako wa kisasa (CV)
• Barua ya Wadhamini wawili wapite Serikali ya Mtaa; pamoja na utambulisho wako wa Makazi
• Maombi yatumwe kupitia barua pepe hr@gininvestment.com au yaende kwa mkono ofisi za Gin Investment – Dar es Salaam – Kinondoni, HUGO House Ghorofa ya 3 kuanzia tarehe ya leo.
• Waombaji wenye nia na watakaokidhi vigezo wataalikwa kufika ofisi za GIN INVESTMENT wa ajili ya usahili siku ya JUMANNE tarehe 25.08.2026.